Hatua 5 muhimu za kufuata kabla ya kuanzisha shamba la vitunguu
Hatua 5 muhimu za kufuata kabla ya kuanzisha shamba la vitunguu
Fahamu kuhusu zao la Vitunguu.
Vitunguu ni zao kubwa linalolimwa na kutumika kwa wingi sehemu mbalimbali duniani kutokana na ladha yake katika chakula. Zipo aina mbalimbali za vitunguu, kulingana na rangi kama vile vyekundu, vyeupe na njano. Katika jamii ya vitunguu pia yapo mazao kama iliki na vitunguu saumu.
1. HALI YA HEWA NZURI KWA KILIMO CHA VITUNGUU:
Vitunguu hupendelea hali ya hewa yenye baridi, kiasi cha nyuzi joto 13 hadi 25. Baridi ikifika nyuzi joto 6 au chini zaidi vitunguu huwa na shingo nene na ndefu na hutoa maua. Unyevu angani kiasi cha 70% na kiasi cha mm 750-1000 za mvua huhitajika kwa kipindi chote cha uzalishaji. Ili kupata mavuno bora mwanga wa jua kiasi cha masaa 12 ama zaidi huitajika.
2. MAHITAJI YA MBEGU NA AINA YA UGONGO UNAOFAA ZAIDI KWA KILIMO CHA VITUNDUU MAJI:
Mahitaji ya mbegu: Kiasi cha mbegu kinachotakiwa kusiwa/kuatikwa/kuoteshwa katika eneo la mita mraba moja ni gramu tano, sawa na kijiko kidogo cha chai. Kiasi cha kilo 2- 2½ ya mbegu za chotara zinahitajika kwa ekari moja ya vitunguu.
Aina ya udogo: Udongo wa tifutifu wenye mboji na kichanga usiotuamisha maji wenye tindikali (pH 5.5-6.9) ni mzuri kwa kilimo cha kitunguu.
Endelea kufuatilia makala za kilimo cha vitunguu katika blog hii.
Je, sasa unafahamu kwa ufupi kuhusu kilimo cha vitunguu? Tuandikie maoni yako