Magonjwa hatari kwenye kilimo cha nyanya

 Magonjwa hatari kwenye nyanya

 

I. Bakajani Wahi/tangulia

II. Bakajani chelewa

III. Bakajani chelewa




 


 

1.  Bakajani Wahi/tangulia. 

Ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia kipindi cha mvua na hali ya hewa ya joto.

 


 

 

Dalili 

·a.  Madoa madogo madogo yenye rangi nyeusi au rangi ya kahawia

yanayo zungukwa na rangi ya njano kwenye majani hasa ya chini.

·b.  Madoa/makovu kwenye matunda na shina.

·c.  Miche midogo kwenye kitalu inaposhambuliwa hunyauka na kufa.

·d.  Miche mikubwa hudondosha majani na kunyauka

 

Udhibiti

·a.  Tumia mbegu na miche bora.

·b.  Hakikisha usafi wa shamba kwa kuondoa majani yaliyoathirika na

ng’oa masalia ya mazao na kuchoma moto mara moja baada ya kuvuna.

·c.  Safisha vitendea kazi kuua vijidudu.

·d.  Zingatia kilimo cha mzunguko wa mazao.

·e.  Tumia viuatilifu sahihi kama Mancozeb, Metalaxyn, Chlorothanonil na

vya asili ya Kopa kwa kufuata maelekezo ya wataalamu

 

 

 

 

2.  Bakajani chelewa

Ni ugonjwa wa ukungu na hatari sana hasa katika kipindi cha mvua na baridi ya

wastani. Joto linapokuwa nyuzi 18 au chini yake hutokea haraka.

 

 


 

 

Dalili 

·a.  Mabaka makubwa yenye majimaji kwenye matunda shina na majani.

·b. Mimea inaposhambuliwa na ugonjwa huu hufa katika kipindi kifupi.

 

Udhibiti

·a.  Zingatia kilimo cha mzunguko wa mazao na panda kwa nafasi inayo

shauriwa kitaalam ili kuwe na hewa ya kutosha.

·b.  Punguza matawi kubaki moja au mawili kuruhusu mzunguko mzuri wa

hewa.  Funga mimea katika fito.

·c.  Ondoa masalia ya mazao shambani mara moja baada ya mavuno

kupunguza vimelea shambani.

·d.  Tumia viuatilifu sahihi kama Mancozeb, Metalaxyn, Chlorothanonil na

vya asili ya Kopa kwa kufuata maelekezo ya wataalamu

 

 

 

3. Mnyauko Bakteria 

Ni ugonjwa hatari wa mnyauko unaosababishwa na bakteria jamii ya Ralstonia  

solanacearum na hutokea zaidi wakati wa joto na hali ya unyevunyevu katika

udongo.

Masalia ya ugonjwa huu yaweza kubaki kwenye udongo na masalia ya mimea kwa

zaidi ya mwaka mmoja. Ugonjwa husambazwa kwa matone ya mvua, wanyama,

maji ya kunywesha, mbegu na vipandikizi, upepo na dhana za kilomo.

 


 

 

Dalili

·a.  Mmea husinyaa wakati kuna unyevu wa kutosha ardhini ukianzia

kwenye ncha za matawi au majani machanga.

· b. Ukikata shina na kupasua katikati, kuna mwozo laini wakati mwingine

unatoa harufu mbaya.

·c.  Mara nyingine mmea hujaribu kutoa mizizi kwenye shina juu ya mizizi.

 d. Ukiweka kipande cha shina kilichokatwa katika glasi ya maji baada ya

dakika 30 au zaidi maji hubadilika rangi na kuwa kama maziwa.

 

Udhibiti

· a. Tumia aina ya nyanya yenye kustahimili mashambulizi.

· b. Tumia mzunguko wa mazao wa muda mrefu, hasa kwa kuhusisha

mazao jamii ya mtama, mpunga au mikunde.

·c.  Panda nyanya zilizoungwa au kubebeshwa na mche mama

unaostahamili ugonjwa.

·d.  Matumizi ya mbolea ya kutosha kama samadi, vunde na mboji

hupunguza tatizo.

·e.  Safisha vifaa vyote vinavyotumika shambani kwa kiua vijidudu kama

jiki kabla ya kutumia vifaa hivyo kwenye shamba lingine.

·f.  Teketeza (choma au fukia mbali) masalia na mimea yote ilioathirika.

·g.  Epuka kutumia maji mengi sana wakati wa umwagiliaji na jaribu

kukwepa matumizi ya maji yanayopita kutoka mashamba yaliothirika

Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url