Zifahamu mbinu 5 za kulima PilIipili hoho kibiashara.


1. Fahamu asili,faida  za kimwili na kibiashara na matumizi  ya pilipili hoho.

PILIPILI HOHO AU PILIPILI MBOGA ni zao muhimu la mboga linalopendwa na kutumiwa na watu wengi .

Aina za pilipili hoho.

Zipo aina tatu za pilipili hoho;

i. zenye rangi ya kijani

ii. zenye rangi nyekundu

iii. zenye rangi ya manjano

Kati ya hizi za kijani hutumiwa kwa wingi zaidi nchini kuliko na zile za rangi nyekundu na njano ambazo hutumika katika hoteli za kitalii na kuuzwa kwenye masoko maalumu (super markets).

picha ya pilipili hoho


Faida za  kimwili na kibiashara na matumizi  ya pilipili hoho

a. kwa kupika na saladi ili kuongeza ladha, rangi, harufu na kuboresha muonekano wa chakula.  

b. Hupatia mwili virutubisho kama vitamin A na C.

c. Hutumika pia kutenegeneza vipodozi.

2. Hali ya hewa nzuri  na udongo unayofaa kwa kilimo cha Pilipili hoho/mboga.

a. Pilipili hoho hustawi vizuri maeneo yenye hali joto la nyuzi za sentigredi 20 hadi 25. Hali joto chini ya nyuzi za sentigredi 16 kwa masaa 120 (siku tano) mfululizo husababisha kuwa na utengenezaji mdogo wa matunda na matunda yasiyo na mbegu wakati joto zaidi ya nyuzi joto za sentigredi 30 husababisha upotevu wa maji kwa wingi katika mmea.

b. Pilipili hoho hustawi karibu kwenye udongo wa aina zote wenye rutuba, kina, husio tuamisha maji bali uwezo mzuri wa kuifadhi maji. Udongo wa kichanga uliorutubishwa vizuri hufaa sana katika maeneo yenye hali ya baridi kwa sababu ya kuwa na tabia ya kupata joto kwa urahisi na hivyo kufanya mizizi kukua vizuri katika joto linalostahili. Udongo wenye tindikali nyingi huzorotesha ukuaji wa pilipili hoho hivyo udongo mzuri kwa pilipili hoho ni ule wenye tindikali kati ya pH 6.0 – 6.8.

3. Maandalizi ya mbegu,shamba na namna ya upandaji miche ya pilipili hoho.

a. Mbegu  Kiasi cha gramu 130 za mbegu au mbegu 15000 huhitajika kuweza kupanda kwenye shamba la ukubwa wa  ekari moja.

shamba lililo tayari kupandwa hoho


b. Maandalizi ya Shamba. Tengeneza matuta yenye kina cha sentimita 30 hadi 45.  Matuta haya yawe katika upana wa mita 1 kutoka kati ya tuta na tuta endapo umwagiliaji kwa njia ya mifereji utatumika, na mita 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta endapo umwagiliaji wa matone utatumika.

c.Upandaji.  Miche ya pilipili hoho/mboga huhamishwa baada ya kukaa kwenye kitalu kwa siku 28-35. Kabla ya kupandikiza miche, shamba sharti limwagiliwe maji na kuwa na unyevu wa kutosha na si tope.

 Pima mashimo ya kupandia kwa kutumia kipimo na kisha toboa mashimo.  Chambua miche kulingana na ukubwa, yaani mikubwa ya kati na midogo na kuweka kila moja katika kundi lake. Kuchambua miche kulingana na ukubwa kuna faida kwani miche yote huweza kuwa katika nafasi nzuri na kuzaa vizuri pasipo kubanwa na miche mingine endapo miche inayotofautiana ukubwa itachanganywa pamoja.



katika mashimo na anza kupanda miche mikubwa na ikiisha panda yenye ukubwa wa kati na mwisho panda midogo. Panda mistari miwili kwenye matuta katika mfumo wa kupishana kulia na kushoto (zigi-zaga) kwa nafasi ya sentimita 40 kutoka shina hadi shina na hivyo kuwa na kiasi cha miche hadi 15000 kwa hekari. Wakati wa kupanda hakikisha upandaji unafanyika haraka baada ya kuweka mbolea kianzio kungali na ubichi ili kuzuia kuwepo kwa sehemu za hewa  kati ya mizizi na udongo na hivyo kuharakisha uchipuaji na ukuaji wa mizizi mipya.

4. Matumizi sahihi ya mbolea(lishe) kwa mimea ya  Pilipili hoho au Pilipili mboga.

a. Mbolea Weka viganja viwili vya mkono vya samadi iliyoiva katika shimo la kupandia kisha changanya na udongo kupata mchanganyiko mzuri.

 Kwa mbolea ya kupandia kama DAP weka kizibo kimoja cha soda katika kila shimo la kupandia kisha fukia mbolea kwa tabaka dogo la udongo kabla ya kupandikiza mche.



 Mimea katika hatua hii  huhitaji kiwango kikubwa cha madini ya chokaa kwa ajili ya kujenga mfumo wa mizizi na kiasi kidogo cha naitrojen kwa ajili ya ukuaji. Hivyo waweza kutumia mbolea ya NPK kama mbadala wa DAP.

 Wiki 3 baadaye, weka mbolea ya NPK. Zingatia ushauri wa wataalam ili kuhakikisha rutuba ya kutosha ya udongo, mbolea ya NPK yaweza kuwekwa mara 2, 3 au zaidi. Endapo umwagiliaji wa njia ya matone utatumika, mbolea mbalimbali zaweza kutumika na kuwekwa mara nyingi na kwa urahisi zaidi.

ZINGATIA:

Mbolea iwekwe umbali wa sentimeta 5 kutoka mmea ulipo. Hili kuepuka kuunguza mmea kwa mbolea.

 

5.Uvunaji Pilipili hoho/mboga za kijani hukomaa baada ya siku 60 na za rangi nyekundu ama njano siku 75 ama zaidi. 



Uvunaji hufanyika mara mbili kwa juma kwa kuzingatia ukubwa wa matunda ama rangi ya kuiva vizuri kwa hoho nyekundu na njano.

Kilimo ni fursa kilimo ni ajira, karibu kwenye kilimo cha pilllipili hoho

Je, una swali lolote?. Tuandikie maonii yako


Next Post Previous Post
No Comment
Add Comment
comment url